AfyaMtandao | Msaada | Wasiliana nasi | Maoni
Tafuta :    
 Mwanzo  | Kuhusu AfyaMtandao  | Habari  | Matukio  | Huduma za Afya  | Maswali Mrudio(FAQ)  | Afya Akaunti  | Links   25th July 2008
                                 
    Magonjwa, jinsi ya kuzuia na kujikinga   Makala za Afya kutoka kwa wataalamu wa afya   Maswali na majibu kuhusu masuala ya afya   Afya Yako na jinsi ya kuiboresha   Afya Katika Picha na maelezo  
                                 
 
 Historia
 Utawala
 Tulipo
 Shughuli Zetu
 Jiunge nasi
 Wasiliana nasi

 

 
      
Mahali Ulipo:  » Mwanzo » Afya Akaunti

Historia

www.Afyamtandao.org  ni  mtandao  wa kompyuta  ulioanzishwa na  Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) kwa lengo la kuunganisha hospitali zote za CSSC katika mtandao wa  tarakilishi ili kuwezesha ukusanyaji, uhifadhi na upashanaji wa taarifa  na ubadilishanaji wa uzoefu na maarifa miongoni mwa watumishi wa afya  na wadau wengine wa sekta ya afya.

Mradi huu ambao umeanzishwa kwa ufadhili wa  Taasisi ya Kimataifa ya Uholanzi ya Mawasiliano na Maendeleo (IICD) ni sehemu ya mkakati wa  CSSC wa kuimarisha  ufanisi katika utoaji wa huduma za kinga na tiba katika  hospitali zake kote nchiini kwa kutumia teknolojia hii ya habarí na mawasiliano (TEKNOHAMA).

Ni katika muktadha huo wa kuongeza ufanisi  na kuimarisha shughuli zake  za utafiti, ushauri  elekezi,,ushawishi na uratibu  ndiyo maana CSSC iliamua kuanzisha  Mradi wa Afyamtandao kwa ajili ya Sekta ya Afya  pamoja na CSSC Public Website kwa ajili ya mawasiliano na umma na dunia kwa jumla.Aidha, pamoja na mitandao hiyo ipo pia  CSSC Intranet ambayo imeanzishwa mahsusi kwa ajili ya kuimarisha mawasiliano  ndani ya CSSC pamoja na taasaisi zake kwa kutumia tekinolojia hii ya kisasa.

Chanzo cha www.Afyamtandao.org  ni Mkutano  wa Pamoja wa   Washikadau wa Sekta ya Afya na  Sekta ya Teknolojia ya  Habarí na Mawasiliano  uliofanyika  mjini Mwanza,Februari  2005 kujadili namna ya kuwezesha matumizi ya  TEKNOHAMA katika mfumo wa taarifa za uendeshaji wa shughuli za afya katika ngazi ya Wilaya.

Mkutano huo uliandaliwa kwa pamoja na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, CSSC na Tume ya Taifa ya Sayansi na Tekinolojia (COSTECH) kwa ushirikiano wa IICD na Netherlands Catholic Organization for Relief and Development Aid (CORDAID).


Mkutano huo ndio uliozaa mipango na maandalizi ya miradi ya ushirikiano  miongoni mwa wadau hao kwa lengo la  kushajiisha  matumizi ya TEKNOHAMA katika kuleta mapinduzi ya kitekinolojia kwenye sekta ya afya.

Ingawa mradi wa Afyamtandao umeanzishwa na CSSC, matumizi yake ni kwa ajili ya washikadau wote wa sekta ya afya ndiyo maana katika Katiba yake mradi huu una kipengere cha Uanachama na vikao vya Wamiliki na  Washikadau ambavyo ndivyo vitakavyoelekeza kuhusu  sera na uendeshaji wake

CSSC ni chombo kilichoundwa mwaka 1992  kwa pamoja kati ya Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) na Baraza la Kikristo Tanzania(CCT) kwa lengo la Kusimamia  huduma za afya na elimu zinazotolewa na Makanisa hapa nchini. CSSC ilisajiliwa  Januari 1993 na mwaka 1994 ikaandikishwa chini ya Sheria ya Wadhamini.

CSSC ni chombo kikubwa zaidi cha Dini hapa Afrika Mashariki kwa sifa kwamba kina Dayosisi na Majimbo 83 na kinamiliki na kuendesha  asilimia 40 ya huduma a afya na asilimia 24 ya huduma za elimu zitolewazo hapa nchini. Habarrí zaidi kuhusu CSSC zinapatikana katika  tovuti kwa anuani:  www.cssc.or.tz

 

 

   
 
Haki zote zimehifadhiwa ©2007 AfyaMtandao.