Jiunge na AfyaMtandao ili kuwa mwanachama ambapo wanachama wetu wamegawanyika katika makundi matatu ambayo ni;
Wanachama washiriki (Corporate members)
Kundi hili la Wanachama linajumuisha watu kutoka idara za serikali kuu na zile za Mitaa,Mashirika yasiyo ya kiserikali,Mashirika ya Dini,Mashirika ya Wataalam yakijumuisha sekta binafsi za Afya.Watumiaji wote wa huduma ya TEKNOHAMA ni wanachama washiriki.
Wanachama wataalamu
Hawa ni wafanyakazi wa Afya wanaojumuisha Wataalamu wa Afya kutoka moja kwa moja kwenye sekta ya Afya na Wataalamu wa TEKNOHAMA.
Wanachama waanzilishi
Kundi hili linaundwa na waanzilishi wa Afyamtandao ambao ni Tume ya Kikristo ya huduma za jamii (CSSC).