Shughuli Zetu
Kazi kuu
(i) Kuwajibika na mahitaji ya watumishi/wafanyakazi wa Afya na kufanya tathimini kwa kubadilishana maarifa,uunganishaji na huduma ya TEKNOHAMA.
Kushirikishana maarifa
(ii) Kuunda jukwaa ambalo watumiaji wa TEKNOHAMA wataweza kuwa na mtandao wa kubadilishana maarifa na kushirikishana uzoefu
(iii) Kujenga na kuendeleza jumuiya ya wataalam wa Afya kwa njia ya mtandao.
Huduma ya TEKNOHAMA
(iv) Kutoa msaada wa vifaa vya TEKNOHAMA na huduma kwa gharama nafuu ikilinganishwa na kiwango cha soko lililopo sasa.
(v) Kutoa msaada wa kiufundi wa TEKNOHAMA na kwa muda unaotakiwa kwa wanachama wake.
(vi) Kutoa mafunzo yfa TEKNOHAMA kwa wanachama na wale ambao siyo wanachama wake.
Miradi maalum
(vii) Kuanzisha miradi ya maendeleo ambayo inajumuisha; masomo,utafiti na ushauri katika maeneo yote ya mifumo ya taarifa na matumizi yake.Maeneyo hayo yanajumuisha; huduma ya tiba kwa njia ya TEKNOHAMA (Telemedicine),Mifumo ya uhifadhi wa taarifa za afya (HMIS),mafunzo kazini kwa njia za Elektroniki na jumuiya ya wataalamu.
(viii) Kupendekeza,kuendeleza na kutoa suluhisho la kitaalamu la TEKNOHAMA.
(ix) Kuweka kiunganishi/viunganishi kwa watoaji wa huduma ya TEKNOHAMA.
(x) Kuchangia maendeleo ya jopo la washauri wa TEKNOHAMA na kuimarisha muongozo wa watoaji huduma ya TEKNOHAMA
(xi) Kuwa na Tovuti na kutoa huduma ya kutengeneza na kuendeleza tovuti.
(xii) Kujishughulisha na shughuli zinazoingiza pato ili kuwezesha malengo yaliyotanjwa kutekelezwa