AfyaMtandao | Msaada | Wasiliana nasi | Maoni | English Version
Tafuta :    
 Mwanzo  | Kuhusu AfyaMtandao  | Habari  | Matukio  | Huduma za Afya  | Maswali Mrudio(FAQ)  | Afya Akaunti  | Links   5th February 2012
                                 
    Magonjwa, jinsi ya kuzuia na kujikinga   Makala za Afya kutoka kwa wataalamu wa afya   Maswali na majibu kuhusu masuala ya afya   Afya Yako na jinsi ya kuiboresha   Afya Katika Picha na maelezo  
                                 
 
 Historia
 Utawala
 Tulipo
 Shughuli Zetu
 Jiunge nasi
 Wasiliana nasi

 

 
      
Mahali Ulipo:  » Mwanzo » Afya Akaunti

Utawala


Petro Masatu Pamba

Mratibu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Tume (CSSC). Anasimamia shughuli zote za mawasiliano ya Mfumo wa kompyuta (ICT).Pia anasimamia na kuratibu shughuli zote za miradi ya AfyaMtandao na Mfumo wa Rasilimali watu Tanzania. Kazi yake ni kuhakikisha kuwa mawasiliano ya Mtandao wa Kompyuta yanakwenada vizuri, Kubuni njia mbadala ambazo zitasaidia Tume kuwa na mfumo wa kisasa zaidi katika Teknolojia ya habari na mawasiliano.Kusimamia miradi ya mfumo wa Kompyuta (AfyaMtandao & Rasilimali watu) ili kuleta ufanisi kwa Tume na wadau wake. Taaluma yake ni Mtaalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT)

Renatus John Sona

Afisa habari (Content  Officer) katika Tume ya Kikristo ya huduma za jamii, anahusika katika kuitangaza Tume kwa njia ya habari na taarifa mbalimbali zinazohusu Tume kwa wadau na jamii kwa ujumla.Anatoa habari kwa njia ya Newsletter, kuweka taarifa katika tovuti ya AfyaMtandao na CSSC, pia anahusika na uzalishaji wa Video kupitia kitengo cha "Media production" na kuandaa mikutano ya ushirikishanaji maarifa na uzoefu wa kazi kwa wadau wa afya wanaotumia mfumo mpya wa Teknolojia ya habari na Mawasiliano (ICT).Taaluma yake ni Mwanahabari katika Mawasiliano ya umma.

Mathayo Josephat

Afisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(ICT Officer), anahusika na shughuli za mifumo ya Kompyuta, mahitaji na ushauri kuhusu  TEKNOHAMA, kwa wale wanaohitaji kuunganishwa na Teknolojia hiyo kupitia Tume ya Kikristu ya huduma za jamii (CSSC).Pia anahusika na shughuli za mradi wa mfumo wa Rasilimali watu Tanzania kwa kusaidia ufungaji na usimamizi wa mfumo huo kwa wadau wa afya wa taasisi za dini na wale wanaotoa huduma kwa faida.Kabla ya kuanza kufanya kazi CSSC, alikuwa nafundisha shule ya Teknolojia ya habari na mawasiliano ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UCC).

Joyce Benedict

Mtendaji wa Ofisi (Office Management Secretary) anahusika na shughuli zote za ofisi katika kuhakikisha kuwa mafaili na nyaraka mbalimbali zinatunzwa vizuri, matayarisho ya mikutano na upangaji wa ofisi katika utaratibu unaotakiwa.

Ernest Itwana

Ni System Administrator,anashughulika na mambo ya kiufundi kama vile;kutatua matatizo katika Sytem,Kompyuta ,(trouble shooting) kufanya service na tathimini kwa wale wanaohitaji kuunganishwa na mfumo wa Kompyuta (Need assessment).

Maua Sume

Ni Mhasibu wa Mradi wa Rasilimali watu Tanzania, anahusika kuhakikisha kuwa masuala yote yanayohusu uhasibu yanafanyika vizuri. Kabla ya kujiunga na CSSC alikuwa anafanyakazi AMREF Mwanza. Anashahada ya usimamizi wa Biashara kutoka Chuo Kikuu cha Mt. Augustine cha Tanzania. 

 

 

   
 
Haki zote zimehifadhiwa ©2007-2012 AfyaMtandao.