AfyaMtandao | Msaada | Wasiliana nasi | Maoni | English Version
Tafuta :    
 Mwanzo  | Kuhusu AfyaMtandao  | Habari  | Matukio  | Huduma za Afya  | Maswali Mrudio(FAQ)  | Afya Akaunti  | Links   9th September 2010
                                 
    Magonjwa, jinsi ya kuzuia na kujikinga   Makala za Afya kutoka kwa wataalamu wa afya   Maswali na majibu kuhusu masuala ya afya   Afya Yako na jinsi ya kuiboresha   Afya Katika Picha na maelezo  
                                 
 
 Habari
 Habari za Kale

 

 
      
Mahali Ulipo:  » Mwanzo » Habari

Habari


Print page  
elearning

eLearning kwa Maendeleo ya Sekta Afya

Tume ya Kikristu ya Huduma za Jamii (CSSC) kupitia mradi wa AfyaMtandao kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Mawasiliano na Maendeleo (IICD),imefanya Warsha ya Masomo kwa njia ya TEKNOHAMA (eLearning) kwa lengo la kuboresha sekta ya Afya nchini. Bw Bandio wa TCMA akitoa maelekezo kwa washiriki wa warsha.

Warsha hiyo ya siku moja ilifanyika hivi karibuni katika ukumbi wa baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC)-Kurasini Dar es salaam.

Lengo la Warsha hiyo iliyohusisha washiriki kutoka katika Taasisi za Afya nchini ilikuwa kujifunza kuhusu elearning jinsi inavyofanya kazi na kubadilishana utaalamu katika kuboresha na kuendeleza taaluma hiyo nchini Tanzania.

Katika warsha hiyo washiriki walijadili mambo muhimu ambayo yanapaswa kupewa kipao mbele ili kuzidi kuboresha huduma hiyo.Mambo hayo ni pamoja na kupandisha madaraja wahusika wa sekta hiyo kwenda kiwango cha juu,kuhamasisha wadau wa Afya kuhusu faida ya masomo hayo,kuainisha maeneo husika ya mafunzo,walengwa na mapato, na kuendeleza taaluma hiyo katika maeneo yote ya nchi.

Baadhi ya waratibu wa miradi walielezea miradi yao. Bw Petro Pamba Mratibu wa AfyaMtandao aliezea kuhusu AfyaMtandao jinsi inavyofanya kazi na mafanikio iliyoyapata tangu ilipoanzishwa Januari 2008,Bw.Dennis Mazali Mratibu wa eLearning aliuelezea mradi huo kwa washiriki jinsi unavyofanya kazi na changamoto zinazoukabili mradi huo.Naye Bi. Miep Lenoir kutoka shirika la IICD linalofadhili miradi hiyo aliwasilisha jinsi ambavyo Shirika lao linavyoshiriki kikamilifu katika kuboresha huduma za Afya kwa njia ya TEKNOHAMA.

 

Imewekwa: 24th Feb 09 na Renatus J Sona

 

 

   
 
Haki zote zimehifadhiwa ©2007-2010 AfyaMtandao.