|
AfyaMtandao
Kubadilishana Maarifa Miongoni mwa Wataalamu wa Afya. Matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika utoaji na usimamizi wa huduma za Afya nchini Tanzania bado ni mageni.AfyaMtandao inawaleta pamoja watoa huduma za afya,watungaji wa Sera na wadau wa Maendeleo katika kupanua wigo na kubadilishana maarifa katika maeneo mbalimbali ya Afya.   Maeneo haya yanajumuisha;Tibamtandao (Kutibu wagonjwa kwa kupata maelekezo kutoka kwa madaktari wengine kwa njia ya Mtandao),Usimamizi wa utunzaji taarifa kwa njia ya mtandao (HMIS) na Masomo kwa njia ya Kompyuta au Mtandao (e-learning kwa watumishi wa Afya).AfyaMtandao inafadhiliwa na Taasisi ya kimataifa ya Mawasiliano ya nchini Uholanzi (IICD) kwa ushirikiano na Shirika la Swiss agency tangu 2006.
Kujenga jukwaa la kushirikishana uzoefu na hospitali zingine. Mikakati ya kuboresha Mawasiliano katika sekta ya Afya imeenea nchi nzima na kila aina ya hospitali ina mpango wake. Kutokuwa na umoja ikiwa na maana kuwa kutokuwa na sauti za pamoja, makubaliano ya pamoja au majadiliano ambapo mashirika na taasisi zinazotoa huduma ya Afya zinaweza kubadilishana na kujifunza uzoefu ambao watanufaika nao.
AfyaMtandao inajaribu kuziba pengo hilo kwa kujenga jukwaa la majadiliano ambapo wataalamu wa TEKNOHAMA (ICT) katika huduma ya afya wataweza kubadilishana maarifa na kuweka sera kama muongozo katika kazi.Mtandao unasimamia mahitaji kutoka kwa wanachama wake.
Imewekwa: 27th Feb 09 na Renatus J Sona
|