|
Makala za Television
Mafanikio ya huduma za afya kwa njia ya makala za Television Tume ya Kikristo ya huduma za Jamii (CSSC) kupitia mradi wake wa Afyamtandao, inaendesha kitengo maalum “Media Unit” cha kutengeza makala na vipindi mbalimbali vya Television vinavyohusu mafanikio ya utoaji huduma za afya, miradi, makongamano, warsha, semina na matukio mbalimbali ya kijamii.
Lengo la kuwa na kitengo hiki ni kuboresha huduma ya afya kupitia makala mbalimbali za TV zenye kuonyesha mafanikio yanayotokana na sekta hiyo.Mfano katika utoaji huduma za afya kuna baadhi ya hospitali ambazo zimefanikiwa kuboresha huduma hizo kwa kiwango kikubwa hivyo hospitali zingine zitahitajika kujifunza mbinu zilizotumika kuleta mafanikio hayo.
Kwa kutambua hilo AfyaMtandao imetekeleza kwa kutengeneza makala ambazo zinaovyesha mafanikio katika sekta hiyo na ushirikiano baina ya hospitali za makanisa na serikali.
Makala zilizokwisha kutengenezwa na zingine kuzambazwa kwa wadau. Makala ambazo kitengo hicho kimetengeneza mpaka sasa ni kuhusu Tibamtandao jinsi inavyofanya kazi kwa baadhi ya hospitali za kanda ya kaskazini, mafanikio ya utoaji huduma za afya mkoani Rukwa ambayo yanayokwenda sambamba na malengo ya milenia, Mfumo wa kuhifadhi na kusimamia taarifa za afya ngazi ya wilaya kupitia “Software” ya AfyaPro katika mkoa wa Mwanza, na njia ya kuwalea watoto ambao hawajatimiza muda wa miezi tisa ya kuzaliwa maarufu kama “Kangaroo method”njia ambayo inatumiwa na hospitali ya teule ya wilaya ya Sengerema.
Nakala kadhaa za makala hayo zimekwisha sambazwa kwa wadau wa afya na wahisani kwa lengo la kushirikishana maarifa na ujuzi huo kutoka katika hospitali zetu.Wadau wote mnakaribishwa kutumia kitengo hiki ili kutangaza shughuli zenu.
Imewekwa: 27th Feb 09 na Renatus J Sona
|