|
WHO na umakini wa dawa
WHO yataka umakini dhidi ya athari za dawa
Glory Kimath na Victoria Kombe
MWAKILISHI wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ameitaka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuongeza nguvu katika kubaini madhara yanayoweza kusababishwa na dawa mara baada ya kuidhinishwa kwa matumizi ya binadamu.Mwakilishi huyo, Dk Jean Tapko alisema hayo wakati akizindua mpango wa ufuatiliaji wa karibu wa usalama wa dawa mseto ya kutibu malaria aina ya Artemether/Lumefantrine (ALu).
Alisema kuwa kuchukua hatua hiyo kutasaidia mamlaka hiyo pamoja na serikali kupunguza madhara ya dawa hizo kwani tafiti zinaonyesha kuwa gharama zinazolipwa kama fidia ya athari za dawa zinachukua kiasi fulani cha bajeti za afya za mataifa mengi.
Alisema katika mataifa kama Marekani, tafiti za hospitalini zinaonyesha kuwa athari zinazotokana na madawa zinachukua nafasi ya nne hadi ya sita katika kusababisha vifo.
"Matatizo yanayohusu usalama na ubora wa dawa yapo katika mataifa mbalimbali, yakiwemo tajiri na yale yanayoendelea na katika baadhi ya mataifa yametokea maafa makubwa kutokana na matumizi ya dawa ambazo usalama wake haujahakikiwa," alisema.
Alisema kuwa kuwepo kwa taratibu na mifumo bora ya udhibiti ni jambo la msingi ambalo linaweza kuweka usalama na ubora wa dawa ambao utalinda afya za watumiaji.
Mkurugenzi mkuu wa TFDA, Margareth Sigonda alisema lengo la mpango huo mpya ujulikanao kama CEM ni kubaini usalama wa dawa hiyo katika mwili wa binadamu na kwamba mradi huo utagharimu Sh86 milioni.
Sigonda alisema kwa muda mrefu mamlaka hiyo imekuwa ikitumia mfumo ambao watoa huduma za afya hujaza fomu za rangi ya njano katika kufuatilia na kukusanya takwimu kuhusu usalama wa dawa.
Alisema mfumo huo umekuwa na mafanikio madogo na kwamba kwa mwaka walikuwa wanapata takribani ripoti ya matukio kati ya 100 hadi 200 za madhara ambayo wanahisi yamesababishwa na dawa hizo.
Ambapo alisema kuwa kwa wastani wa kiwango cha utoaji taarifa za madhara ya dawa duniani kwa mfumo huo kinakadiriwa kuwa asilimia tatu ya matarajio.
Sigonda alisema mpango huo, ambao utachukua miaka miwili, utatekelezwa katika hospitali za rufaa, vituo vya afya na zahanati zilizo mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro na Mwanza na kwamba kujumuishwa kwa mikoa mingine kutatagemea
Imewekwa: 18th Mar 09 na Renatus J Sona
|