AfyaMtandao | Msaada | Wasiliana nasi | Maoni | English Version
Tafuta :    
 Mwanzo  | Kuhusu AfyaMtandao  | Habari  | Matukio  | Huduma za Afya  | Maswali Mrudio(FAQ)  | Afya Akaunti  | Links   9th September 2010
                                 
    Magonjwa, jinsi ya kuzuia na kujikinga   Makala za Afya kutoka kwa wataalamu wa afya   Maswali na majibu kuhusu masuala ya afya   Afya Yako na jinsi ya kuiboresha   Afya Katika Picha na maelezo  
                                 
 
 Habari
 Habari za Kale

 

 
      
Mahali Ulipo:  » Mwanzo » Habari

Habari


Print page  
Ushawishi na utetezi

 

Ushawishi na utetezi katika sekta ya afya.


Ushawishi na utetezi katika sekta ya afya una nafasi kubwa katika zana nzima ya  uboreshaji sekta hiyo nchini Tanzania. Akiwasilisha mada inayohusu ushawishi na utetezi (Lobbying and advocacy), kwenye mkutano mkuu wa jumuiya ya kikristu Tanzania (CCT), uliyofanyika mjini Dodoma hivi karibuni, Mkurugenzi wa Tume ya Kikristu ya huduma za jamii (CSSC) Dk. Adeline Kimambo amesema lengo la ushawishi ni kuwa na sera zenye kulenga mipango bora itakayoboresha huduma hiyo. Mkurugenzi wa Tume ya Kikristo ya huduma za jamii (CSSC) Dk.Adeline Kimambo

Pamoja na kuwa na sera, suala la kushiriki kikamilifu katika kutekeleza na kufuatilia utekelezaji wa mpango mkakati lazima lipewe kipau mbele, kwani makanisa yana mchango mkubwa katika kutekeleza hilo kwa kuwashirikisha kikamilifu waumini wake pamoja na serikali kuunga mkono juhudi hizo kwa manufaa ya ustawi wa taifa. Katika suala la ushawishi  ni muhimu pia kuangalia uwezo wa wananchi kwani nao wana nafasi ya pekee katika kuchangia huduma hii.

CSSC kama tume ya pamoja katika kuratibu huduma ya afya inafanya kazi kubwa katika kuhamasisha makanisa  na Serikali hususani halmashauri kwa malengo ya ushawishi, kuwajengea uwezo watumishi (capacity building), ushauri na huduma.

Aidha Dk. Kimambo amebainisha kuwa, suala la ushawishi na utetezi ni kwa ngazi zote kuanzia kwenye halmashauri za wilaya hadi ngazi ya taifa, kwani gharama za huduma ya afya ni wajibu wa kila mmoja ikiwa ni pamoja na utaratibu wa serikali kuwezesha mashirika ya dini kuwa na watumishi wa kutosha, madawa na vifaa.

Sekta ya afya kwa upande wa makanisa inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na baadhi ya watumishi wa taasisi hizo kuhama na kwenda kujiunga na  taasisi za serikali, na baadhi ya watumishi wa halmashauri kuwa na uelewa hafifu kuhusu zana ya ushirikiano baina ya sekta ya umma na binafsi (PPP), uhaba wa watumishi (idadi, taaluma) na fedha.

Askofu Bruno Ngonyani kutoka jimbo katoliki la Lindi alifungua mkutano huo kwa kusoma neno lililokuwa na ujumbe mkuu unaosema; “muwe na nia moja, msilipizane mabaya”.


 

Imewekwa: 12th Jun 09 na Renatus J Sona

 

 

   
 
Haki zote zimehifadhiwa ©2007-2010 AfyaMtandao.