AfyaMtandao | Msaada | Wasiliana nasi | Maoni | English Version
Tafuta :    
 Mwanzo  | Kuhusu AfyaMtandao  | Habari  | Matukio  | Huduma za Afya  | Maswali Mrudio(FAQ)  | Afya Akaunti  | Links   9th September 2010
                                 
    Magonjwa, jinsi ya kuzuia na kujikinga   Makala za Afya kutoka kwa wataalamu wa afya   Maswali na majibu kuhusu masuala ya afya   Afya Yako na jinsi ya kuiboresha   Afya Katika Picha na maelezo  
                                 
 
 Habari
 Habari za Kale

 

 
      
Mahali Ulipo:  » Mwanzo » Habari

Habari


Print page  
CSSC na mkataba wa huduma ya afya

 

CSSC na mkataba wa huduma ya afya (Service Agreement).
Tume ya kikristo ya huduma za jamii (CSSC), kwa kushirikiana na Serikali imeendelea na mikutano ya kuhamasisha hospitali za makanisa na halmashauri za wilaya kusaini mkataba wa utoaji huduma ya afya (Service Agreement) kama moja ya mkakati wa maboresho ya huduma ya afya na ushirikiano baina Serikali na watoa huduma za afya binafsi.DK.Kisanga na DK.Ndamugoba wa CSSC wakiwa katika moja ya mikutano ya Service Agreement

Mkataba huo ambao  umeanzishwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wa afya umelenga kuongeza upatikanaji wa huduma ya haraka hasa ya mama na mtoto mpango ambao unakwenda sambamba na malengo ya millennia.Imeripotiwa kuwa akina mama wajawazito 578 wamekuwa wakipoteza maisha yao kati ya vizazi hai 100,000 kwa mujibu wa Utafiti wa Idadi ya Watu na Afya Tanzania.

Mkataba huu utawezesha watoa huduma za afya binafsi kupata fedha kutoka serikalini kupitia Halmashauri za wilaya kwa lengo la kutoa huduma ya afya bure kwa watoto waliyo chini ya umri wa miaka mitano, wakina mama wajawazito na wasiojiweza ili kuokoa vifo vinavyotokana na kada hizo,

Akielezea mkataba huo Dk. Obeline Kisanga wa wizara ya afya amesema, mpango huu ni njia pekee yenye muelekeo wa maisha bora kwa kila mtanzania ambao utawezesha hospitali za mashirika ya dini kupata watumishi ambao wataajiliwa na serikali kupitia halmashauri za wilaya na kwenda kufanya kazi katika taasisi hizo na mishahara yao ikilipwa na Serikali kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa huduma bora zinazokwenda sambamba na sera ya taifa ya kuboresha huduma ya afya nchini.

Dk. Kisanga ameshauri halmashauri kuwa na mpango endelevu wa kusaidia hospitali binafsi mfano kutoa vifaa na madawa ambayo yatasaidia kuboresha huduma badala ya kufikiria kujenga vituo vingine vya afya sehemu ambazo tayari taasisi za dini zina hospitali.

Akielezea mafanikio yaliyopatikana kwa baadhi ya hospitali ambazo tayari zimeingia katika makubaliano ya pamoja ya  ushirikiano wa huduma ya afya baina ya Serikali na taasisi za dini, Ofisa anayeshughulikia masuala ya Sera (CSSC), Dk Godwin Ndamugoba amesema, “mkataba huu (Service Agreement) umesaidia vituo binafsi kutengewa fedha na halmashauri huska na kujenga uaminifu katika matumizi yake kwani mafanikio yanaonekana”.

Serikari kuu na zile za halmashauri zimekuwa zikichangia kwa kupeleka watumishi “Seconded staff” kwa msaada kufanya kazi katika hospitali za taasisi na baadhi ya huduma kama vile Chanjo, mama na mtoto kufanyika huko.

CSSC kwa kushirikiana na wizara ya afya imekuwa mstari wa mbele kuelimisha taasisi za dini pamoja na halmashauri kujua faida zitokanazo na mkataba huo ili ziweze kuutekeleza.

 

Imewekwa: 4th Aug 09 na Renatus J Sona

 

 

   
 
Haki zote zimehifadhiwa ©2007-2010 AfyaMtandao.