AfyaMtandao | Msaada | Wasiliana nasi | Maoni | English Version
Tafuta :    
 Mwanzo  | Kuhusu AfyaMtandao  | Habari  | Matukio  | Huduma za Afya  | Maswali Mrudio(FAQ)  | Afya Akaunti  | Links   9th September 2010
                                 
    Magonjwa, jinsi ya kuzuia na kujikinga   Makala za Afya kutoka kwa wataalamu wa afya   Maswali na majibu kuhusu masuala ya afya   Afya Yako na jinsi ya kuiboresha   Afya Katika Picha na maelezo  
                                 
 
 Habari
 Habari za Kale

 

 
      
Mahali Ulipo:  » Mwanzo » Habari

Habari


Print page  
Tathimini ya TEKNOHAMA hospitali ya Bulongwa

 

Tathimini ya TEKNOHAMA hospitali ya Bulongwa

Timu ya CSSC- AfyaMtandao hivi karibuni ilifanya tathimini ya TEKNOHAMA katika hospitali ya Bulongwa kwa lengo la kuboresha huduma ya afya inayotolewa hospitalini hapo kwa njia ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEKNOHAMA).Katika zoezi hilo lililofanyika kwa wiki nzima, ilifahamika kuwa, hospitali hiyo ina Kompyuta za kutosha na baadhi ya maeneo tayari yana Soketi  ambazo zinaweza kuunganisha Kompyuta hizo na mfumo maalumu wa kuhifadhi taarifa za wagonjwa (AfyaPro au Care2x). Maeneo hayo yaliyo na Soketi ni yale ya wagonjwa wanaokuja kutibiwa na kuondoka (Outpatient rooms) na yale ya wagonjwa wanaolazwa (Ipatient rooms), pia ofisi za utawala na uhasibu.Bw.Petro Pamba akitoa maelezo kwa wafanyakazi wa hospitali

Tathimini hiyo pia imeonyesha kuwa, hospitali hiyo pia ina chumba maalumu cha Mtandao (Internet) ambacho kina Kompyuta tatu na kinatumiwa na watumishi wa hospitali hiyo kupata taarifa mbalimbali za afya.

Pamoja na kuwa na  Kompyuta chache, hospitali hiyo inakabiliwa na tatizo la kuwa na watumishi wachache walio na uelewa wa kutumia Kompyuta, hivyo ilipendekezwa kuwa watumishi wengi wapewe mafunzo ya Kompyuta kwa kuanza kufundishwa  hatua ya awali za namna ya kutumia Kompyuta.Pia katika tathimini hiyo, hospitali hiyo ilishauriwa kuanzisha tovuti yake ambayo itatumika kujitangaza na watu wengi kufahamu huduma  zitolewazo na hospitali hiyo na kuajiri mtalaamu wa ufundi atakayesaidia kutatua matatizo mbalimbali ya Kompyuta.

Hospitali ya Bulongwa ni moja kati ya hospitali kongwe ambayo imefanikiwa katika kutoa huduma bora ya afya nchini Tanzania.Miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na kutoa huduma ya Mtandao (Internet) kwa wakazi wa kijiji cha Bulongwa, kuongeza idadi ya wataalamu wa tiba kati yao ni madaktari wawili wa kigeni, na kujenga kituo cha watoto yatima.Pamoja na mafanikio hayo, hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na miundombinu ya kufika hospitalini hapo kuwa hafifu, kutokuwa na gari maalumu la wagonjwa (Ambulance).Hospitali hiyo iko katika kijiji cha Bulongwa, wilaya ya Makete mkoa wa Iringa na ilianza kama Zahanati mwaka 1946 na ilipanda na kuwa hospitali mwaka 1968.


 

Imewekwa: 10th Sep 09 na Renatus sona

 

 

   
 
Haki zote zimehifadhiwa ©2007-2010 AfyaMtandao.