AfyaMtandao | Msaada | Wasiliana nasi | Maoni | English Version
Tafuta :    
 Mwanzo  | Kuhusu AfyaMtandao  | Habari  | Matukio  | Huduma za Afya  | Maswali Mrudio(FAQ)  | Afya Akaunti  | Links   9th September 2010
                                 
    Magonjwa, jinsi ya kuzuia na kujikinga   Makala za Afya kutoka kwa wataalamu wa afya   Maswali na majibu kuhusu masuala ya afya   Afya Yako na jinsi ya kuiboresha   Afya Katika Picha na maelezo  
                                 
 
 Habari
 Habari za Kale

 

 
      
Mahali Ulipo:  » Mwanzo » Habari

Habari


Print page  
Mfumo wa DHMIS umekuwa kivutio ECSA Arusha

 

Mfumo wa DHMIS wawavutia washiriki wa mkutano wa ECSA Arusha

Mfumo wa kuhifadhi na kusimamia taarifa za afya za wilaya kwa njia ya Kompyuta (DHMIS), umewavutia washiriki wengi wa mkutano wa 3 wa nchi za jumuiya ya mashariki, kati na kusini mwa bara la Afrika (ECSA) uliyofanyika mjini Arusha hivi karibuni na baadhi yao wameonyesha nia ya kuhitaji msaada huo ili waanze kuutekeleza mradi.

Washiriki wa mkutano wa 3 wa ECSA wakiwa katika picha ya pamojaMfumo huo umekuwa kivutio kwa wengi baada ya washiriki kuoneshwa filamu ya mfumo huo jinsi unavyofanyakazi.Filamu hiyo ya dakika kumi iliyotengenezwa na CSSC-AfyaMtandao kwa ufadhili wa Shirika la afya duniani ofisi ya Tanzania (WHO) inaonyesha faida ambazo zinapatikana na aina ya mahitaji muhimu yanayohitajika katika kuanza kutumia mfumo huo.Pia filamu hiyo inaonyesha watumishi wa afya wakielezea mfumo huo jinsi unavyowarahisishia kazi ikilinganishwa na ugumu waliokuwa wakiupata kabla ya kuanza kutumia mfumo huo.

Baada ya kutazama filamu hiyo washiriki hao, waliuelezea mfumo huo kuwa ni mzuri na unarahisisha kazi na wakapongeza hatua ya CSSC kutengeneza filamu hiyo sambamba na mradi ambao unatekeleza mfumo huo jijini Mwanza.

Mmoja wa washiriki hao, Profesa Steven Kinoti alisema mfumo huo unawawezesha watawala wa vituo vya afya kupata ripoti safi na sahihi ambazo zinawasaidia kuleta mabadiliko kwenye vituo vyao.

Akizungumza kwenye mkutano huo mtaalamu wa ufundi wa DHMIS, Bw. Deogratias Kattonyella alisema katika kuwajengea uwezo watumishi hao wa vituo vya afya, mradi umetoa mafunzo kwa baadhi ya watumishi ya namna ya kutatua matatizo madogo (trouble shooting) na namna ya kuhifadhi taarifa kwa njia mbadala endapo umeme utakatika.Mafunzo hayo yamesaidia kiasi kikubwa na hakuna matatizo makubwa yanayotokea.

Mkutano huo wa 3 wa ECSA ulihudhuliwa na washiriki kutoka nchi za Kenya, Uganda, Malawi, Zimbabwe, Zambia, Lesotho, Swaziland, Afrika ya kusini na wenyeji Tanzania.

 

 

Imewekwa: 1st Oct 09 na Renatus sona

 

 

   
 
Haki zote zimehifadhiwa ©2007-2010 AfyaMtandao.