AfyaMtandao | Msaada | Wasiliana nasi | Maoni | English Version
Tafuta :    
 Mwanzo  | Kuhusu AfyaMtandao  | Habari  | Matukio  | Huduma za Afya  | Maswali Mrudio(FAQ)  | Afya Akaunti  | Links   8th September 2010
                                 
    Magonjwa, jinsi ya kuzuia na kujikinga   Makala za Afya kutoka kwa wataalamu wa afya   Maswali na majibu kuhusu masuala ya afya   Afya Yako na jinsi ya kuiboresha   Afya Katika Picha na maelezo  
                                 
 
 Habari
 Habari za Kale

 

 
      
Mahali Ulipo:  » Mwanzo » Habari

Habari


Print page  
Suala la Rasilimali watu ni tatizo

 

Suala la Rasilimali watu ni tatizo-Dk.Adeline Kimambo

Dk. Adeline Kimambo mkurugenzi wa CSSCImeelezwa kuwa sekta binafsi kwa kushirikiana na Serikali inajukumu kubwa la kutatua tatizo la Rasilimali watu ili kutoa huduma bora isiyokuwa ya ushindani baina ya watoa huduma wa sekta binafsi na Serikali.

Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa Tume ya Kikristo ya huduma za jamii (CSSC) Dk.Adeline Kimambo kwenye mkutano wa uzinduzi wa kamati maalumu itakayosimamia mradi wa Rasilimali watu Tanzania ambao umeanza kutekelezwa na Tume hiyo kupitia kitengo cha AfyaMtandao.

Dk. Kimambo ameeleza kuwa suala la Rasilimali watu ni tatizo kutokana na  kuwa hakuna mfumo ambao unatumika kutunza takwimu za watumishi hivyo inakuwa ngumu kwa hospitali kujua idadi ya watumishi iliyonao, kada na elimu zao.


CSSC kwa kushirikiana na wadau wengine ikaona kuna  umuhimu wa kutatua tatizo hilo kwa kuanzisha mfumo ambao utawezesha kutambua na kuzipata takwimu sahihi za watumishi hivyo ikaona ni bora kuanzisha mradi huu ili hospitali za taasisi za dini, Serikali na zile za binafsi zianze kutumia mfumo huo.

Picha ya washiriki wa mkutano wa rasilimali watuAidha Dk.Kimambo amebainisha kuwa ili kufanikisha azima hii ya kuwa na mfumo huo, ushirikiano wa pamoja baina ya Serikali, taasisi za dini na sekta binafsi ni muhimu sana katika kuboresha huduma ya afya kwa kufanikisha utekelezaji wa mradi.

Mradi wa Rasilimali watu ni wa miaka minne na umeanza kutekelezwa na CSSC mwezi Septemba mwaka jana, na mwaka wa kwanza ni wa uhamasishaji kwa wadau kuelewa mfumo wenyewe jinsi utakavyofanya kazi ambapo CSSC inashirikiana na wadau wengine wa afya ambao ni umoja wa watoa huduma ya afya binafsi (APHFTA) na Baraza la waislamu Tanzania (Bakwata). Mkutano wa uzinduzi wa kamati hiyo ulifanyika Kibaha Pwani na mradi huu unafadhiliwa na watu wa Marekani kupitia shirika la IntraHealth-Tanzania.

 

Imewekwa: 6th Jan 10 na Renatus sona

 

 

   
 
Haki zote zimehifadhiwa ©2007-2010 AfyaMtandao.