AfyaMtandao | Msaada | Wasiliana nasi | Maoni | English Version
Tafuta :    
 Mwanzo  | Kuhusu AfyaMtandao  | Habari  | Matukio  | Huduma za Afya  | Maswali Mrudio(FAQ)  | Afya Akaunti  | Links   9th September 2010
                                 
    Magonjwa, jinsi ya kuzuia na kujikinga   Makala za Afya kutoka kwa wataalamu wa afya   Maswali na majibu kuhusu masuala ya afya   Afya Yako na jinsi ya kuiboresha   Afya Katika Picha na maelezo  
                                 
 
 Habari
 Habari za Kale

 

 
      
Mahali Ulipo:  » Mwanzo » Habari

Habari


Print page  
Hospitali ya Dareda na huduma ya Ukimwi

 

Mafanikio ya huduma ya ukimwi katika hospitali ya mission Dareda

Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya DaredaMafanikio katika sekta ya afya ni pamoja na kuzuia kabisa maambukizi mapya na kupunguza vifo vitokanavyo na ugonjwa wa ukimwi, mpango unaokwenda  sambamba na malengo ya milenia katika kupambana na Ukimwi, Malaria na Kifua kikuu. Hospitali ya Dareda  imekuwa mstari wa mbele katika kupiga vita maambukizi mapya ya Ukimwi, hali iliyochangia kuleta mafanikio makubwa katika wilaya ya Babati na wilaya zingine za mkoa wa Manyara

Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali hiyo Dk. Stephen Ammi anasema, Katika kukabiliana na tatizo la HIV/AIDS, hospitali ya Dareda ina mradi wa ukimwi ambao unasimamia na kuratibu shughuli zote katika kutoa huduma kwa waathirika wa ukimwi na uhamasishaji kwa wanajamii ili wajitokeze kupima afya zao kwa ufadhili wa Shirika la SolidarMed na mpango wa taifa wa kudhibiti ukimwi (NACP), hali ambayo imechangia kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo katika wilaya ya Babati.


Dk. Ammi anaendelea kusema,  ndani ya mradi wa Ukimwi kuna kitengo cha huduma endelevu kinachoshughulika na utoaji wa  dawa za kurefusha maisha kwa walioathirika na ukimwi (CTC) sambamba na huduma ya kuzuia maambukizi ya Virus vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT).

Moja ya mafanikio ya mradi wa ukimwi hospitalini hapo ni kutoa huduma ya mkoba (outreach services) katika vijiji mbalimbali vilivyomo ndani na nje ya wilaya Babati kwa ushirikano wa wanajamii na Serikali za vijiji kwa lengo la kuwarahisishia wagonjwa wanaotoka maeneo y a mbali katika vijiji vya Riroda, Babati vijijiji na Endasaki.

Mbali na huduma ya mkoba kutolewa pia elimu ya  kuhamasisha watu wajitokeze kupima afya zao imetolewa katika vijiji mbalimbali, ikiwemo vikundi maalumu vya vijana mashuleni, wanawake na wanaume.Pia semina ya ukimwi imetolewa kwa viongozi wa vijiji kwa kata 3 za Dareda, Dabili na Arri.

Dada Veronika muathirika wa Ukimwi akiwa na Bi.Claudia wote wakazi wa Endasaki-Hanang Tangu mradi wa ukimwi uanze kutekelezwa katika hospitali ya Dareda, kumekuwepo na mafanikio makubwa ikiwemo kuongezeka kwa watu wanaojitokeza kupima na kufahamu afya zao na wanaobainika kuwa wameambukizwa wanashauriwa kuingia katika mpango wa kutumia dawa, kwa vile wengi wao wameelewa umuhimu wa kupima. Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha mwaka 2008 jumla ya watu 5916 walijitokeza kupima kwa hiyari virusi vya Ukimwi na 159 walibainika kuwa wanamaambukizi ya Ukimwi. 2009 waliojitokeza ni 9458 na waliobainika na maambukizi ni 191.  Mafanikio ya huduma ya Ukimwi katika hospitali ya Dareda yanatokana na ushirikiano uliyopo baina ya hospitali yenyewe, Serikali, wanajamii pamoja na wadau wengine wa afya kama Tume ya kikristo ya huduma za jamii (CSSC).

Hospitali ya Dareda imeanzishwa na wamisionari wa Shirika la Maria (Medical Missionaries of Mary) mwaka 1948 na inamilikiwa na Kanisa katoliki jimbo la Mbulu. Miongoni mwa huduma inazotoa ni kwa wagonjwa wa ndani (IP) na wagonjwa wa nje (OPD) na ina jumla ya watumishi 203.

 

Imewekwa: 16th Feb 10 na Renatus sona

 

 

   
 
Haki zote zimehifadhiwa ©2007-2010 AfyaMtandao.