|
Uwezo wa kukusanya, kuchambua na kutumia taarifa sahihi ni muhimu katika kuwawezesha wafanyakazi wa sekta ya afya kutoa huduma bora kwa ufanisi.Aidha kupatikana kwa taarifa sahihi na kwa wakati ni muhimu katika kuwawezesha waandaaji wa sera kufanya maamuzi sahihi.
Cha kusikitisha ,hali ya sasa sivyo ilivyo.Taarifa zinazokusanywa kwa kutumia karatasi na kalamu zinakabiliwa na upotoshaji, upotevu na uharibifu na zinachukua muda mrefu kuwekwa katika mfumo wa matumizi,hatua nyingine inayohatarisha usahihi wake. Ubora wa huduma za fya zitolewazo unaathiriwa vibaya na matatizo ya mawasiliano na uhaba wa vyazo vya habarí za afya na tiba kama vile majarida. Taasisi za afya za AICT zinakabiliwa na matatizo makubwa ya kupata kwa wakati taarifa sahihi na ni mara chache waandaaji sera wanapata taarifa muhimu za kuwasaidia katika kufanya maamuzi. Uanzishwaji wa Mfumo wa Taarifa za Uendeshaji Huduma za Afya Wilayani una lengo la kutumia Teknohama(ICT) kuimarisha uwezo wa kukusanya, kuchambua na kuhifadhi taarifa za afya katika ngazi ya wilaya kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za afya, kuhakikisha usahihi wa taarifa na hatua zinazochukuliwa pamoja na kuongeza uwajibikaji na kutoa picha sahihi ya mienendo ya afya wilayani. Hali ilivyo sasa Mradi huu ulianza Februari 2006 na unaendelea.Mapitio ya kwanza ya mradi yalifanyika mwishoni mwa Septemba 2006
Muhtasari Afyanet Tanzania imekusudiwa kuwa mtandao unganishi kwa ajili ya sekta ya afya.Utatoa huduma bora kwa wateja na kuziunganisha taasisi za afya kwenye mtandao. Kwa mfano,sekta ya afya Tanzania ina miradi mingi kama vile ile ya malaria na Ukimwi.Kwa sababu kila mradi unajitegemea uratibu katika sekta ya afya unakuwa mgumu kwa sababu ya kukosa ushirikiano na mawasiliano.Kukiwepo na kiungo kimoja cha miradi yote ya sekta ya afya miaradi hii itashirikiana na kuboresha huduma kwa wateja. CSSC inasimamia karibu asilimia 40 ya sekta ya afya hapa nchini.Kuanzishwa kwa Intranet katika CSSC kutasaidia kupanua matumizi ya teknohama(ICT) katika kuimarisha mawasiliano na upeanaji maarifa na taarifa. Kuwapatia elimu viongozi wa makanisa kuhusu teknohama kutasaidia kuharakisha mchakato wa kuanzishwa kwa Afyanet Tanzania na kukubalika kwake.
HIV/AIDS Uelimishaji na ubadilishaji tabia za Vijana VVU/UKIMWI (HIV/AIDS) ni janga la kimataifa. Vijana wengi hasa wa vijijini bado hawana uelewa wa kutosha kuhusu janga hili. CSSC ambacho ni chombo cha makanisa yenye waumini ambao ni sehemu kubwa ya jamii bado haina taarifa na mikakati inayokubalika kwa wadau wake ya kukabiliana na janga hili Teknohama(ICT) ni njia mojawapo ya kuwezesha uandaaji na usambazaji wa taarifa kuhusu namna ya kupambana na ukimwi. Katika mradi huu, vikundi vya wanafunzi vikisaidiwa na wataalamu vinaandaa mikakati ya kuelimishana kwa vijana wa rika mbalimbali pamoja na wazazi wao na waumini wengine kwa jumla. Vielelezo na maigizo ni moja ya njia zinazotumika kutoa elimu hii
Muhtasari KJatika baadhi ya maeneo vijijini,ukeketaji wanawake bado ni mila inayoendelezwa na kuchukuliwa kama kinga dhidi ya magonjwa kama m alaria, homa ya mapafu na ukimwi.Kuwaelimisha wananchi na waganga wa jadi ni njia mojawapo ya kukabiliana na tatizo hili. Tanzania Inter African Committeé (TIAC) inatambua kwamba ingawa dunia imejaa bado elimu ya kutosha ya afya haijafika vijijini. Mradi huu una lengo la kusambaza elimu ya afya vijijini ili kukabiliana na mila potofu zinazodhuru afya za wananchi kama ile ya ukeketaji wanawake.
Elimu kuhusu Afya ya Uzazi
UCHUNGUZI NA TIBA
Muhtasari Mradi huu pia una lengo la kutoa huduma ya uchunguzi wa kidaktari na tiba kwa njia ya mtandao wa kompyuta nchini Tanzania
SERA YA TEKNOHAMA NA MKAKATI WA UTEKELEZAJI WAKE
P6-30.316:MKAKATI WA TEKNOHAMA KWA WANACHAMA WA CSSC
|