Muhtasari Uwezo wa kukusanya, kuchambua na kutumia taarifa sahihi ni muhimu katika kuwawezesha wafanyakazi wa sekta ya afya kutoa huduma bora kwa ufanisi.Aidha kupatikana kwa taarifa sahihi na kwa wakati ni muhimu katika kuwawezesha waandaaji wa sera kufanya maamuzi sahihi. Cha kusikitisha ,hali ya sasa sivyo ilivyo.Taarifa zinazokusanywa kwa kutumia karatasi na kalamu zinakabiliwa na upotoshaji, upotevu na uharibifu na zinachukua muda mrefu kuwekwa katika mfumo wa matumizi,hatua nyingine inayohatarisha usahihi wake. Ubora wa huduma za fya zitolewazo unaathiriwa vibaya na matatizo ya mawasiliano na uhaba wa vyazo vya habarí za afya na tiba kama vile majarida. Taasisi za afya za AICT zinakabiliwa na matatizo makubwa ya kupata kwa wakati taarifa sahihi na ni mara chache waandaaji sera wanapata taarifa muhimu za kuwasaidia katika kufanya maamuzi. Uanzishwaji wa Mfumo wa Taarifa za Uendeshaji Huduma za Afya Wilayani una lengo la kutumia Teknohama(ICT) kuimarisha uwezo wa kukusanya, kuchambua na kuhifadhi taarifa za afya katika ngazi ya wilaya kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za afya, kuhakikisha usahihi wa taarifa na hatua zinazochukuliwa pamoja na kuongeza uwajibikaji na kutoa picha sahihi ya mienendo ya afya wilayani. Hali ilivyo sasa Mradi huu ulianza Februari 2006 na unaendelea.Mapitio ya kwanza ya mradi yalifanyika mwishoni mwa Septemba 2006
|