AfyaMtandao | Msaada | Wasiliana nasi | Maoni | English Version
Tafuta :    
 Mwanzo  | Kuhusu AfyaMtandao  | Habari  | Matukio  | Huduma za Afya  | Maswali Mrudio(FAQ)  | Afya Akaunti  | Links   9th September 2010
                                 
    Magonjwa, jinsi ya kuzuia na kujikinga   Makala za Afya kutoka kwa wataalamu wa afya   Maswali na majibu kuhusu masuala ya afya   Afya Yako na jinsi ya kuiboresha   Afya Katika Picha na maelezo  
                                 
 

 

 
      
Mahali Ulipo:  » Mwanzo » Miradi ya Afya

Miradi ya Afya

Maelezo zaidi
Malezo ya Mradi
Muhtasari
Uendeshaji wa taasisi za afya unakabiliwa na  tatizo la uongozi dhaifu kutokana na uhaba wa watendaji , kuondoka kwa wataalamu  na matumizi hafifu ya taarifa. Taarifa zinazopatikana kutoka kwenye taasisi za afya hazina ubora  na zinawachukua watendaji muda mrefu kuziandaa.Miundombinu ya Teknohama(ICT) iliyoko Tanzania hivi sasa inawezesha baadhi ya taasisi za afya kutumia mtandao wa kompyuta  kuandaa taarifa  za uendeshaji huduma za afya .
Mradi huu unalenga kuandaa mifumo mahsusi ya uendeshaji  huduma za afya kwa ajili ya taasisi za KKKT Mifumo hiyo ya MTUHA itakuwa hususan kwa ajili ya taasisi hizo lakini pia itakuwa  inakidhi viwango na mahitaji ya MTUHA ngazi ya Taifa.
Historia ya mradi Wabia:CSSC
Wamiliki wa Mradi: KKKT
Goal Maendeleo
MTUHA utaleta  mtiririko mzuri wa taarifa  zilizoandaliwa kwa usahihi na kupatikana kwa wakati.Hali hii itawezesha uandaaji wa mipango ya afya kwa uhakika zaidi na uchunguzi wa wagonjwa kufanyika kwa  makini  na haraka zaidi  na kwa hiyo wagonjwa wengi zaidi kuhudumiwa.
Objectives Malengo
Malengo ya mradi ni haya yafuatayo:-
1. Kutengeneza programu mahsusi za kompyuta kwa ajili ya taasisi husika  lakini pia kukidhi mahitaji ya MTUHA-taifa
2. Kuweka kompyuta katika taasisi husika  ili kuwezesha MTUHA kufanya kazi
3. Kuwa na watendaji waliofunzwa namna ya kutumia  MTUHA kwa ufanisi
4. Kuhakikisha kunakuwepo huduma za kiufundi caribú na taasisi.
5. Kuhakikisha kuwa kunakuwa na mawasiliano kati ya waendeshaji wa mfumo huo na watumiaji ili kuhakikisha kuwa mahitaji ya watumiaji yanazingatiwa  na mfumo unaboreshwa kila mahitaji ya kufanya hivyo yanapojitokeza
6. Kuhakikisha kuwa taasisi zote 26 za afya zinahusishwa katika mfumo huo na mwongozo wa namna ya kutumia mfumo huo na huduma za kiufundi na mafunzo kuhusu tekinolojia hii ya kisasa yanapatikana
Target Soko
Wadau wakuu wa mradi huu ni taasisi za afya za KKKT. Ni kwa manufaa ya watoaji huduma za afya kuwa na mfumo makini wa kukusanya taarifa  muhimu za uendeshaji huduma za afya. Ndani ya mfumo huo programu ya MEMS itanufaika  sana  na mradi huu kwani unawezesha matumizi ya kompyuta  katika kuhakiki mali na usimamizi wake. Ndani ya CSSC,  taasisi za afya zamakanisa mengine zinafuatilia kwa karibú kuona mafanikio ya mradi huu  Wizara ya Afya na Mamlaka za  Afya za Mikoa na Wilaya  zitanufaika na mradi huu kwani zitapata  taarifa  bora zaidi ambazo zitakuwa msingi wa kuanzisha matumizi ya kompyuta  katika uendeshaji wa huduma za afya. Mradi huu utapunguza mianya ya rushwa na ubadhilifu.Waliokuwa wakinufaika na uovu huo watajaribu kuuhujumu mradi huu. Kwa hiyo utaratibu wa kutoa motisha na mafunzo ya mabadiliko ya fikra kwa waathirika ni mambo  yanayohitajika. Wabia wa mradi huu wa Managed Health Care Programme(MHCP) watapenda kuuuona unafanikiwa.
Mategemeo Uendeshaji
Huu utakuwa moja ya miradi iliyoko chini ya  Idara ya Afya ya KKKT Timu ya  Uendeshaji wa Mradi ndiyo itakayofanya maaamuzi yote muhimu  na Meneja wa Mradi  ndiye atakayehusika na uendeshaji wa siku kwa siku. Matatizo yatakayojitokeza yatapelekwa kwa Mkurugenzi wa Huduma za Afya wa KKKT
Mafaniko Hali Halisi ilivyo sasa
Mradi umeanza.Mafunzo  na maandalizi ya programu za kuendeshea mifumo hiyo inaendelea Warsha kuhusu mabadiliko ya uendeshaji na utendaji kazi ilifanyika Septemba 19-20 2006.
Mfadhili

IICD of the Netherlands

Fedha
Wafadhili wa mradi huu ni IICD, Cordaid na MHCP

Barua pepe mniemi@elct.or.tz
Mradi Unaanza 0000-00-00
Mradi Unaisha 0000-00-00
Anwani ya Jumla KKKT
Simu ya Mezani 0272508855-7
Hali ya Mradi Progessing
Anwani binafsi Dk.Mauri Niemi
Anwani ya shirika KKKT
Mratibu Dk.Mauri Niemi
Gharama N/A
Nyaraka : Chukua waraka


« 

 

 

   
 
Haki zote zimehifadhiwa ©2007-2010 AfyaMtandao.