Muhtasari Gharama za kujiunga katika tovuti bado ziko juu sana hapa Tanzania.Lakini kwa kuungana na kushirikiana katika kununua bandwidth gharama hizo zinaweza kupungua kwa karibú asilimia 40. Taasisi nyingi za afya bado zinakabiliwa na ukata na hazina vyazo vya uhakika vya mapato licha ya kwamba nyingi ya hizo bado hazijaweza hata kujiunga katika mtandao au hata kuanzisha matumizi ya kompyuta katika ofisi zake. Lengo lingine la kuanzishwa kwa mradi huu wa Afyanet ni kwamba iwe chombo kitakachounganisha taasisi za afya katika mazungumzo ya kibiashara ya ununuzi wa bandwidth kwa ajili ya kuuunganisha taasisi hizo kwenye tovuti. Aidha Afyanet itatoa pia huduma za kiufundi kwa wanachama wake na wateja wengine kwa jumla.
|